Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limefanikiwa kufanya maboresho ya mita za luku kwa mikoa ya kanda ya kati na kaskazini.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Makao Makuu TANESCO, Irene gowele amesema zoezi hilo litaanza kufanyika kuanzia Agosti 26, hadi Novemba 24, 2024.
“Zoezi hili la maboresho ya mfumo wa mita za luku sasa ni zamu ya Morogoro, Dodoma, Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga, na maboresho haya yanalenga kuendana na viwango vya mifumo ya LUKU vya kimataifa na kuongeza ufanisi na usalama wa mita za LUKU Nchini,” amesema.
“Na mteja atakaponunua umeme kwa mara ya kwanza kuanzia tarehe hiyi atapokea tarakimu kwenye makundi matatu, kilakundi likiwa na tarakimu ishirini, kundi la kwanza na la pili tarakimu yatakuwa kwaajili ya maboresho na kundi la tatu tarakimu litakuwa ni la umeme ulionunuliwa,” aliongeza Gowele
Hata hivyo, amesema zoezi hilo ni bure na litafanyika mara moja tu kwa mteja na baada ya kufanya hivyo mteja atakuwa amefanya maboresho hayo na ataendelea kupata kundi moja la tarakimu ishirini kila atakapofanya manunuzi ya umeme.
“Shirika linawahimiza wateja wake wote kununua umeme ili kuweza kufanya maboresho hayo kwenye mita zao ambapo ukomo wa zoezi hili katika maeneo yote Nchi nzima ni 24 Novemba 2024 na zoezi hili ni kwa Nchip nzima,”amesema.