Watuhumiwa wanne kati ya sita wanaokabiliwa na kesi ya kubaka na kulawiti ambapo video ya tukio hilo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, wamefikishwa Mahakamani.
Katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dodoma Watuhumiwa hao walisomewa makosa mawili hii leo Agosti 19, 2024.
Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema kosa la kwanza linalowakabili ni kubaka kwa kundi na kosa la pili ni kumuingilia kinyume cha maumbile Binti huyo.
Watuhumiwa hao ni MT. 140105 Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, Amin Lord Lema ,Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi na kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano hadi Agosti 23, 2024.