Serikali Nchini, imesema imejipanga kuudhibiti ugonjwa wa Mpox kwa kuimarisha uchunguzi kwa wasafiri katika mipaka ikiwemo bandari, nchi kavu na viwanja vya ndege, ili kubaini wasafiri wenye dalili za ugonjwa huo.

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Wanahabari kuhusu mwenendo wa Ugonjwa huo ulitangazwa na Shirika la Afya Duniani- WHO.

Amesema Wananchi wasiwe na hofu kwani Tanzania ipo salama hivyo waendelee kushirikiana na Serikali kuhakikisha nchi inaukabili ugonjwa huo.

Agosti 14, 2024 Vituo vya Umoja wa Afrika vya Kudhibiti Magonjwa – CDC, piq vilitangaza rasmi aina mpya ya virusi vya mpox kuwa dharura ya kiafya kwa umma.

CHADEMA watoa tamko kushikiliwa kwa Soka, wenzie
Wananchi wasisitizwa umuhimu wa kutunza Mazingira