Serikali ya Kenya imesema italazimika kurejesha vipengele vya ulipaji kodi ambayo zilifutwa baada ya kuibuka kwa maandamano makubwa hivi karibuni.
Waziri wa Fedha wa Kenya, John Mbadi amesema baadhi ya vipengele hivyo vitarekebishwa, ili kumudu matumizi ya serikali na ulipaji wa mishahara ya walimu.
Mbadi alisema hayo wakati wa mahojiano na kituo cha luninga cha Citizen, huku baadhi ya watu walioshiriki maandamano wakisema wapo tayari kuingia tena mitaani na kuandamana ikiwa jambo hilo litaibuka tena.
Tayari wadadisi wa mambo ya kisiasa wanadai kuwa hatua hi ya Kenya inaweza kuzidisha hatari ya kutokea kwa machafuko zaidi na kutaka viongozi kuwa na fikra chanya ya kimaamuzi.