Lydia Mollel – Morogoro.

Wafanyabiashara wa Halmashauri ya Mji wa Mikumi, wameitaka menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Mikumi kuendelea kudumisha mahusiano mazuri yalipo kati yao na wananchi wa eneo ilo ikiwa ni pamoja na kuwatembelea mara kwa mara na kusikiliza kero wanazokutanazo

Hayo yamejiri mara baada ya uongozi wa Hifadhi ya taifa mikumi kuwatembelea wafanyabiashara wa soko la Green mikumi, na kushirikiana kwa pamoja kufanya usafi wa mazingira ili kupunguza uwepo wa taka katika soko hilo na kuhamasisha utalii wa ndani ikiwa ni wiki ya maandalizi ya kuelekea maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Hifadhi ya Taifa Mikumi.

Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi (ACC), Augustine Masesa.

Abdulkareem Dimoso, ni Mfanyabiashara wa soko la Green,amesema wainaitaji ushirikiano kati ya wahifadhi na wananchi kuendelea kwani itasaidia kutatua kero zilizopo pamoja na kukuza utalii wa ndani.

“Mkuu wa Hifadhi ya mikumi amefanya jambo jema kulikumbuka soko letu ambalo lilisaauliwa kwa muda mrefu,atukudhani kama tutakumbukwa juu ya swala zima la usafi,lakini mkuu wa hifadhi amelifikiria hili katika kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya hifadhi ya mikumi na kuja kufanya usafi katika soko la Green mikumiambalo ndio soko kuu la mikumi.”

“Na sisi tupo tayari kuwapokea wageni watakaokuja kututembelea ila tunaomba ushirikiano uzidi kudumu katika ya hifadhi na wananchi,waje watutembele kama walivyokuja leo na kuzungumza na sisi ili wajue kero tunazozipata na wao watueleze kero zao tushirikiane kukuza utalii wetu,” alisema Abdulkareem.

Amina Abdala, ambaye pia ni Mfanyabiashara katika soko hilo, alisema mazingira ya soko hayakuwa salama kwa afya ya binadamu kutokana na uwepo wa uchafu, lakini anaishukuru menejimenti ya Hifadhi ya Mikumi kwa kushirikiana nao kufanya usafi na kuweka mazingira hayo kuwa safi na salama.

“Hapo awali mazingira ya soko letu alikuwa rafiki na salama kwa afya zetu lakini tunawashukuru watu wa hifadhi kwakuja hapa na kushirikiana pamoja na sisi kufanya usafi kwenye mazingira yetu kwa sasa mtu akifika hapa ataona utofauti mkubwa,na mazingira yamekuwa salama kwa wateja wetu,” alisema Amina.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa zoezi hilo, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya Mashariki, Jonh Nyamuhanga alisema lengo la kushirikiana na wananachi ni kuwahamasisha wananchi kuendelea kutunza na kuhifadhi maliasili mbalimbali zilizopo nchini ili kukuza zaidi utalii kwa kuweka mazingira yanayozunguka hifadhi hiyo katika hali ya usafi.

“Siku ya leo tumekuja katika eneo hili lengo likiwa ni kufanya usafi pamoja na kuhamasisha ulinzi wa maliasili tulizonazo pamoja na kuhamasiha utalii, kwa faida ya sasa na vizazi vinavyokuja,hivyo tumeamua kushirikiana na wananchi wa mikumi kufanya shughuli za usafi ili eneo hili liwe mfano katika shughuli zetu za uhifadhi na maswala yote ya utalii,” alisema Kamishna Nyamuhanga.

Naye Mkuu wa Hifadhi ya Mikumi Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi (ACC), Augustine Masesa amesema wataendeleza ushirikiano kati yao na wananchi wanaozunguka eneo hifadhi hiyo ikiwa ni muendelezo wa huduma walizokuwa wakitoa hapo awali.

“Sisi kama hifadhi ya taifa Tanapa tunatoa huduma kwa jamii hususani kuvisaidia vikundi vya kinamama,wengine wanafuga kuku kuna wengine wanafuga ng’ombe na pia kuna vijana ambao ri kati ya hifadhi na wananchi pamoja na kuamasisha utalii wa ndani.

Arsenal yatikisa kikosi bora cha msimu
Foden awapiku Haaland na Rodri tuzo za PFA