Washtakiwa wanne wanaokabiliwa na kesi ya ubakaji kwa kundi na ulawiti, hii leo Agosti 21, 2023 wamefikishwa tena katika Kituo cha Utoaji Haki, Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma kwa siku ya tatu mfululizo.

Washtakiwa hao kupitia Kesi nambari 23476 ya mwaka 2024, wanadaiwa kumbaka kwa kundi na kumlawiti binti aliyejitambulisha kuwa anatokea eneo la Yombo lililopo jijini Dar es salaam.

Washtakiwa hao MT. 140105 Clinton Honest Damas (Nyundo), Amin Lord Lema, Nickson Idala Jackson na C.1693 Playgod Edwin Mushi wamefikishwa na pamoja na Washtakiwa wa kesi nyingine.

Agosti 20, 2024, mmoja wa Mawakili wa Washtakiwa hao, Meshack Yonah Ngamando alisema “Shauri leo lilikuwa linakuja kwa ajili ya kusomwa kwa hoja za awali, lakini lilikuwa limepangwa pia kwa ajili ya kuendelea ambapo hoja za awali zilisomwa.”

SMZ yapanga kuweka mkazo uzalishaji wa Mwani
Dawa ya Kaswende iliyoniponya baada ya kuumwa sana!