Kufuatia Maafisa watano wa Polisi nchini Kenya wamefikishwa mahakamani wakituhumiwa kumsaidia mshukiwa wa mauwaji na mahabusu 12 kutoroka kwenye kituo kimoja cha Polisi mjini Nairobi, msako umeanza kuwatafuta waliotoroka.

Waendesha mashitaka wameiomba mahakama kuwazuilia polisi hao kwa wiki mbili zaidi, ili kuwawezesha maafisa kukamilisha uchunguzi kuhusu kisa hicho kupitia simu zao njia zingine za kipolisi.

Polisi ilisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa watu wa ndani waliwasaidia washukiwa kutoroka huku msako unaendelea kuwakamata waliotoroka.

Waliotoroka ni Collins Jumaisi, aliyekamatwa Julai kuhusiana na mauaji ya karibu wanawake sita ambao miili yao ilipatikana ikiwa imefungwa kwenye mifuko ya plastiki na kutupwa kwenye dampo ambaye Wakili wake aliiambia Mahakama kuwa aliteswa na kulazimishwa kukiri tuhuma hizo.

Othman: Hoja za ACT zimewaelemea
Ahmed Ally afunguka kinachowanyima furaha wanasimba