Wanafunzi wa Shule tano za Msingi na moja ya Sekondari katika ya Msoga wameanza kambi maalumu ya kujiandaa na mitihani yao inayotaraji kufanyika hivi karibuni.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata hiyo Hassani Mwinyikondo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi ya kata wakati akikabidhi mchango wa vyakula Afisa Elimu Msingi Miriamu Kihiyo, hatua inayolenga kuwawezesha kufanya vizuri kwenye mitihani yao.

Mtoro Tamla na Abdul Tengwe Mwalimu Mkuu shule ya Changa walishukuru kwa msaada huo, huku Omary Kisina Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Msoga akiuelezea kwamba sio wa kisiasa, bali unalenga kuendeleza elimu.

Wakulima fuateni ushauri wa Wataalamu - TMA
Tukio la 'Afande' wa ulawiti, ubakaji lazidi kushika moto