Udadisi ni nini? Udadisi ni tabia ya kuchunguza kitu au jambo kwa kina na mara nyingi Wanasayansi ndio wadadisi wazuri kwa maana wao huchunguza kwa kina na umakini.
Wengi wao hufuata kanuni na kutafuta ushahidi na kwa udadisi wao wamejikuta wakistawisha maisha ya binadamu.
Hata hivyo, kuna udadisi wa kawaida na mwingine usio wa kawaida, kwa mfano udadisi wa kawaida mtu hudadisi kwa njia rahisi, tofauti na ule usio wa kawaida ambapo mtu asipokuwa makini anaweza hata kufa.
Udadisi unahitaji umakini sana ingawa tendo hujitokeza mapema utotoni ambapo wengi wa Watoto hupenda kufuatilia mambo kwa kina bila kutambua kuwa udadisi mwingine ynaweza kuwadhuru.
Hata hivyo, kuna tatizo katika udadisi kwani unapozidi na kufuatilia mambo yasiyo na maana (kwa mfano umbeya), huo utakuzuia usijue mambo ya maana mwishowe unapata kilema cha akili.
Udadisi unaweza kukupa ushujaa, au hata tuzo lakini pia unaweza kubadilisha maisha yako kama ambavyo ilitokea Septemba 10, 1957 kwa mpiga picha William C. Beall wa Washington Daily News.
Yeye siku hiyo alipewa kazi ya kuchukua picha za gwaride lililoandaliwa na Chama cha Wafanyabiashara wa China na kwa umakini wake akiwa kwenye msafara huo, pembeni aliona mtoto mdogo aliyevutiwa na kwata za Gwaride hilo.
Yule dogo alijitosa bila kujali Umatilla watu ili aangalie kwa karibu, lakini akadakwa na askari Polisi mmoja mrefu na ambaye alimueleza kwa upole kwamba si salama kusogelea gwaride.
Mpiga picha anasema, “ghafla, nikaona nikipiga picha itakuwa na matokeo, nikalenga kamera yangu, na kubofya kitufe cha kupiga picha lakini sikujua kama ingeleta matokeo makubwa.”
Picha iliyopatikana ilifikishwa Chumba cha Habari, hapo Mhariri akaona ni ya tukio kubwa na iliyobeba ujumbe unaogusa jamii na ilipochapishwa ilimletea William C. Beall Tuzo ya kifahari ya Pulitzer mwaka 1958.
Uzuri wa kiini cha udadisi wa mtoto na hujumuisha hisia ya mshangao, umedumu katika kumbukumbu za historia ya upigaji picha, hivyo katika eneo lako la kazi endelea kuwa mdadisi, mbunifu au hata mfuatiliaji wa mambo yaliyo ya maana, nina uhakika utakula mema ya nchi.