Klabu ya Simba imeendelea kufanya vyema michuano ya Ligi kuu NBC baada ya kuibuka na ushindi wa maba 4-0 dhidi ya Fountain Gates ya Manyara mchezo uliopigwa dimba la KMC Complex.

Bao la kwanza la Simba liliwekwa kimiani na Edward Charles Balua akimalizia pasi kutoka kwa Ahoua dakika ya 13. Bao la pili liliwekwa kimiani na Steven Mukwala akimalizia pasi kutoka kwa Shomari Kapombe dakika ya 44. Mchezo ulikwenda mapumziko Simba wakiongoza kwa mabao 2-0.

Kocha Fadlu alifanya mabadiliko kwa kuwatoa Shomari Kapombe nafasi yake ikichukuliwa na Kelvin Kijili,Valentino Mashaka akichukua nafasi ya Mukwala,Awesu Awesu akimpisha Kibu Denis. Mabadiliko haya yalizaa matunda kwa upande wa Simba wakijipatia bao la tatu kutoka kwa Ahoua akimalizia pasi mpenyezo kutoka kwa Mohammed Hussein dakika ya 58. Valenttino Mashaka alikamilisha ushindi wa mabao manne dakika ya 80kwa kumalizia pasi iliyotoka kwa Jean Ahoua.

Jean Ahoua aliibuka nyota wa mchezo huo kwa kufunga bao 1 na kutengeneza mengine mawili. Nyota jhuyu mpaka sasa amekwisha tengeneza mabao 3 katika mechi mbili za ligi kuu.

Supa Sub Valentino Mashaka anaongoza orodha ya ufungaji bora akiwa na mabao 2 kwenye mechi mbili alizocheza.

Klabu ya Simba imeanza vyema mbio za ligi kuu kwa kujikusanyia alama 6 na mabao 7 ya kufunga kwenye michezo miwili waliyocheza walifungana na Singida Black Stars wenye mabao 3 na alama 6.

Gamondi hana wasiwasi na kikosi chake
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 26, 2024