Chelsea wana nia ya kumnunua winga wa Manchester United Muingereza Jadon Sancho, 24, na huenda wakamjumuisha mshambuliaji wa Uingereza Raheem Sterling, 29, katika mkataba wa kubadilishana wachezaji. (Telegraph – usajili unahitajika)
Chelsea wameanza tena mazungumzo na klabu ya Napoli kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria Victor Osimhen, 25, huku masharti yakiwa mazuri zaidi kwa klabu hiyo ya Uingereza. (Sky Sports)
Kumuuza kiungo wa Scotland Scott McTominay, 27, kwa Napoli kutaimarisha harakati za Manchester United kumnunua kiungo wa kati wa Uruguay Manuel Ugarte, 23, ambaye klabu yake ya Paris St-Germain inataka kumuuza kwa pauni milioni 51. (ESPN)
Crystal Palace wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Arsenal Muingereza Eddie Nketiah, 25, baada ya uwezekano wake wa kuenda Nottingham Forest kutibuka. (Athletic – usajili unahitajika
Nottingham Forest wamewasilisha ofa ya tatu ya £29.7m kwa Feyenoord kwa ajili ya kumnunua mshambuliaji wa Mexico Santiago Gimenez, 23, ambayo itakuwa rekodi ya juu ta mauzo kwa klabu hiyo ya Uholanzi. (Fabrizio Romano)
Napoli wana matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Scotland Billy Gilmour kutoka Brighton, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya wiki hii. (Fabrizio Romano
Kiungo wa kati wa Celtic na Denmark Matt O’Riley, 23, anafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu kabla ya kuhamia Brighton. (Sky Sports)
Manchester City wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Iceland Orri Oskarsson mwenye umri wa miaka 19 kutoka FC Copenhagen. (Athletic – usajili unahitajika)
Manchester City wako tayari kupokea ombi la kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Matheus Nunes, 25, baada ya kiungo wa zamani wa Ujerumani Ilkay Gundogan, 33, kurejea kutoka Barcelona. (Football Insider)
West Ham wako tayari kumtoa kiungo wa kati wa Uingereza James Ward-Prowse, 29, kabla ya Ijumaa ambayo ni siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji. (Team Talk)
Liverpool huenda wakamnunua mlinzi wa Sporting Lisbon wa Ureno Goncalo Inacio, 22, huku beki wa Bayer Leverkusen na Ecuador Piero Hincapie, 22, pia akinyatiwa. (Team Talk)