Kaimu Kocha mkuu wa timu ya Taifa Hemed Suleimani amekitaja kikosi cha wachezaji 23 watakaoingia kambini tarehe 28 Agosti kujiandaa na mechi za kufuzu AFCON 2025 nchini Morroco. Taifa stars itacheza mchezo wake wa kwanza wa kufuzu michuano hiyo dhidi ya Ethiopia tarehe 04 Septemba na mchezo wa pili utachezwa tarehe 10 septemba dhidi ya Guinea.
Majina ya Mbwana Samatta,Aishi Manula na Simon Msuva yamekosekana kwenye kikosi hicho hivyo hawatakuwemo kwenye mechi hizo. Hawa hapa wachezaji walioitwa na kocha huyo.
Klabu ya Azam FC imetoa wachezaji watano kwenye kikosi hicho ambao ni Lusajo Mwaikenda ,Nathaniel Chilambo,Pascal Msindo ,Adolf Mtasingwa na Feisal salum.Klabu ya Dodoma jiji imetoa mchezaji mmoja ambaye ni Mshambuliaji Wazir Junior.Simba wametoa wachezaji watatu ambao ni Mohammed Hussein Ally Salim na Edwin Balua. Golikipa Yona Amos ametajwa kutoka Pamba jiji akiungana na Cyprian Kachwele kutoka Vancouver Whitecaps,Novatus Dismas kutoka Goztepe,Abdul Malik Zakaria kutoka Mashujaa na Hussein Semfuko kutoka Coastal Union.
Klabu ya Yanga imetoa wachezaji 7 ambao ni wengi zaidi kuliko klabu yoyote. Majina ya wachezaji hao ni Abutwalib Mshery,Dickson Job,Ibrahim Hamad,Bakari Nondo Mwamnyeto,Nickson Kibabage,Mudathir Yahaya na mshambuliaji Clement Mzize.