Naibu kamishna wa Polisi Kitengo cha udhibiti Makosa yanayovuka Mipaka, DCP. Daniel Nyambabe amewakabidhi askari wa kike Bendera ya Taifa kwa ajili ya Kwenda nchini Marekani kushiriki mafunzo kwa askari wa kike Duniani katika jimbo la Chicago Nchini humo kuanzia Septemba 1-5, 2024.
Akikabidhi bendera hiyo hii leo Agosti 26,2024 Makao Makuu Ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam, DCP. Daniel Nyambabe amesema Askari hao wanakwenda kuhudhuria mafunzo hayo ya Dunia ambayo yanahusisha askari wa kike na wasimamizi wa sheria ambapo amewasisitiza kuzingatia mafunzo nchini Marekani.
Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaamini kuwa mafunzo wanayokwenda kuyapata yataleta chachu ya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya Jeshi la Polisi huku akibainisha kuwa Jeshi hilo linaamini kuwa washiriki hao ni kielelezo kizuri cha nchi ambapo amewataka kuwa na nidhamu kipindi chote cha mafunzo.
Aidha ameeleza kuwa kuwa ushiriki wa askari wa Jeshi la Polisi katika mafunzo hayo ya Dunia ni uwakilishi wa Nchi ambapo amewataka askari hao Kwenda kulinda na kutunza taswira nzuri ya nchi iliyojengwa kwa muda mrefu na waasisi wa nchi hii.

RCT yawatahadharisha Wakulima wa Mpunga
Hali ya Mazingira: Serikali kukutana na Wadau