Baraza la Mchele Tanzania – RCT, limewatahadharisha Wakulima wa Mpunga nchini kutotumia Mbegu za Mpunga zinazofanyiwa tafiti ambazo hazijathibitishwa na kamati ya Mbegu ya Taifa, ili kuepusha kupata hasara katika kilimo.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa RCT, Geoffrey Rwiza wakati akizungumza na Jukwaa la kilimo cha mpunga Wilaya ya kilosa mkoani Morogoro amesema mbegu hizo zinakuwa bado hazijafikiwa mwisho katika kufanyiwa utafiti.
Awali, Afisa kilimo kutoka Kata ya Mvumi wilayani Kilosa Mwanaharusi Matola ameomba Watafiti wanapofika kwa Wakulima kufanya tafiiti watoe taarifa kuhusu mbegu hizo wanazofanyia utafiti.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Wakulima mpunga Wilaya ya Kilosa, Ramadhani Ndalika ameomba Serikali isaidie Wakulima kumaliza Kero ya ujazaji Mchele kwenye gunia kiasi cha Rumbesa katika zao hilo ili Wakulima wapate tija na taifa lipate mapato.