Boniface Gideon, Handeni – Tanga.

Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya ‘Marafiki wa Maendeleo Handeni'(MMAHA), mwishoni mwa wiki imetoa msaada wa taulo za kujistili kwa Mabinti waliopo kwenye maandalizi ya mitihani ya kidato cha pili na nne lakini pia wametoa sabuni kwa wavulana, shule 8 za secondari zimenufaika zikiwemo, Shule ya sekondari Misima, Handeni Sekondari,Mkata na Segera.
lengo la kutoa msaada huo nikuwasaidia Mabinti na Vijana wa kiume waliopo kwenye maandalizi ya mitihani ya Taifa ya kidato cha pili na nne, kufanya maandalizi ya mitihani ya Taifa kwa utulivu mkubwa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo,Mwenyekiti wa MMAHA ,Mariam Mwanirwa alisema,wao kama wadau wa Maendeleo wilayani humo wameamua kuwasaidia Wanafunzi ambao kwa sasa wapo kwenye maandalizi ya mitihani ya Taifa ya kidato cha pili na nne.

“Taasisi yetu iliameanza kufanya kazi mwaka 2020 na tumekuwa tukitoa misaada mbalimbali katika Sekta za Elimu, Afya na Uchumi.

Wanafunzi wa Shule ya Handeni Sekondari wakifurahia jambo na Viongozi wa MMAHA Mwishoni mwa wiki wakati wa kitoa msaada wa Taulo za kike na Sabuni.

Mchengerwa asikiliza changamoto za Wanafunzi Kigoma
Samatta na Msuva watupwa nje Taifa Stars