Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tamisemi, Mohamed Mchengerwa amesikiliza changamoto za Wanafunzi toka kwa Katibu Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Sayansi Kigoma, Varelia Masele.
Waziri Mchengerwa ametoa fursa hiyo kama sehemu ya kusikiliza changamoto za wanafunzi baada ya kuwa amewasikiliza Viongozi na Walimu wa Shule hiyo.
Katika ziara yake shuleni hapo, Waziri Mchengerwa amefanya ukaguzi wa ujenzi wa majengo mbalimbali yanayoendelea kujengwa shuleni hapo katika kuhakikisha shule hiyo inakidhi viwango vilivyotolewa na serikali katika ujenzi wa shule za sayansi za wasichana nchi nzima.
Katibu huyo Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi wa Shule ya Wasichana, Varelia Masele ni Mwanafunzi wa kidato cha tano, shuleni hapo.

Wafukua miili mitatu ya waliopotea, saba mbaroni
Miradi ya MMAHA yawanufaisha Wanafunzi 1,200