Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango, amelitaka jeshi la polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kuongeza udhibiti kwa magari yanayobeba wanafunzi (School bus) ambayo mengi hayakidhi vigezo vya kutembea barabarani na madereva wake wengi hawana weledi.

Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Jijini Dodomq, alipokua akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani na miaka 50 ya Baraza la Taifa la Usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa jijini Dodoma.

Amesema, jeshi la polisi linapaswa kuongeza udhibiti kwenye mabasi ya shule ambayo yamekuwa yakitumika kubeba wanafunzi lakini mengi hayana sifa ya kutembea barabarani.

“Jeshi la polisi linapaswa kuongeza udhibiti wa mabasi ambayo yamekuwa yakitumika kubeba watoto wa shule kwani mengi hayana sifa ni mabaovu na mengine yanabeba watoa zaidi ya uwezo wake lakini pia madereva wake wengi hawana weledi”,amesema

“Madereva hao wamekuwa wakisababisha ajali za ovyo kama ile iliyotokea Aprili 12 mwaka huu kule Arusha ambapoa wazazi walipoteza watoto wao saba kwa uzembe ninawataka jeshi la polisi kuhahakisha kuwa dereva nayepata leseni lazima awe amekidhi vigezo vyote vya udereva na siyo vinginevyo,” amesema Dkt. Mpango.

Aidha, amesena madereva wote wanaovunja sheria wanapaswa kuchukuliwa hatua kali bila kujali kuwa ni dereva wa serikali au binafasi.

Pia, alilitaka jeshi la polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kuendesha doria za kushitukiza za kufanya ukaguzi wa magari pamoja na weledi wa madereva na wasio kidhi vigezo kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Dkt. Mpango, amesema kwa hali ilivyo sasa kama hatua madhubuti za kudhibiti ajali hazitachukuliwa taafiti zinaonyesha kuwa ajali ndiyo inakuwa chanzo kikuu cha vifo ifikapo mwaka 2030.

“Taifa letu linapoteza nguvu katika kipindi cha mwaka 2023 katika ajali 1,733 vifo ilikuwa ni 1,647 na majeruhi ni 2,716 hivyo kama hatutachukua hatu basi ajali ndiyo itakuwa chanzo kikuu cha vifo ifikapo 2023”alisema

Ameonhezea kwa kusema ajali za pikipiki hivi sasa nchini zinaongezeka ambapo kwa kipindi cha mwaka 2023 ajali zilikuwa 435 ambapo vifo ni 376 ukilinganisha na vifo 332 kwa mwaka 2022.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamad Yusuf Masauni, amesema katika kukabilina na tatizo la ajali nchini wizara imetekeleza miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza hali hiyo.

Amesema moja kati ya miradi hiyo ni pamoja na ule wa miji salama wa kufunga kamera za usalama kwenye miji (Safe City) ambao utekelezaji wake upo katika hatua za mwisho ambapo utakwenda kutekelezwa kwenye majiji ya Dodoma, Arusha, Mwanza na Dar es Saalam.

“Ni matumaini yetu kuwa miradi hii ikikamilika tutakwenda kudhibiti ajali hasa katika maeneo yasiyo na askari kutoka na kamera zitakazokuwa zimefungwa katika maeneo hayo”amesema

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo, alisema moja ya sababu ya kuongezeka kwa ajali barabarani ni makosa ya kibinadamu.

“Baadhi ya madereva hawazingati masuala ya sheria za usalama barabarani hivyo kufanya makosa ya kibinadamu na kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ajali nchini kutokana na hali hiyo Baraza tumeandaa mkakati utakao shirikisha wadau wote na baada ya miezi tutafanya tathimini kuona hali iikoje”. Amesema Masauni

Vilevile, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Cumillius Wambura, amesema katika kukabilina na ajali nchini wametekeleza maagizo mbalimbali ya serikali ikiwemo kufunga mifumo ya kisasa kudhibiti ajali barabarani.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Agosti 27, 2024
Mgonjwa wa 13 apona sikoseli BMH