Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuwekeza zaidi katika sekta ya elimu kwa kujenga miundombinu bora na kuboresha maslahi ya walimu ili mafanikio yanayopatikana yaongezeke kila mwaka.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Ikulu, Mjini Unguja, kwenye hafla maalum ya chakula cha mchana aliyowaandalia wanafunzi wa kidato cha nne na sita waliofanya vizuri katika mitihani yao ya taifa ya mwaka 2023 (kidato cha nne) na mwaka 2024 (kidato cha sita) kwa upande wa Unguja.
Amesema, Serikali itaweka kipaumbele kuimarisha miundombinu, kuajiri walimu zaidi hasa kwa masomo ya sayansi, na kusimamia maslahi ya walimu ili kuwaongezea motisha ya kufanya kazi kwa ufanisi huku akielezea kufarijika kwake na mafanikio yaliyopatikana, ikiwemo ongezeko la idadi ya wanafunzi waliopata daraja la kwanza..
Rais Dkt. Mwinyi pia amebainisha kuwa Serikali inakusudia kuongeza fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya juu, na ametoa wito kwa wanafunzi kutumia fursa hiyo kujiendeleza zaidi.

Augustine Okrah alamba dili jingine baada ya Yanga
Tetesi za Usajili Duniani Agosti 27