Kama tunavyofahamu, Mwanaume ni binadamu wa jinsia ya kiume na kabla ya kuitwa Mwanaume huwa anaitwa Mtoto wa kiume au mvulana. Ila akimpata mtoto hapo ataitwa kwa kawaida Baba, jina lenye heshima kubwa katika utamaduni wa aina nyingi. Halafu akipata wajukuu, anajulikana pia kama babu.
Lakini Mwanaume ana tabia zake za kipekee katika upande wa mwili, nafsi na roho na tofauti kati yao na Wanawake hujitokeza kwa namna mbalimbali za kiutendaji.
Hata hivyo, tofauti nyingi zinategemea pia utamaduni, kwa sababu mara nyingi watu wamepanga shughuli au namna ya maisha tofauti kwa kuangalia Wanaume na Wanawake, hivyo watu wamezoea kuchukua matokeo ya mapatano haya kama jambo la kimaumbile hata kama ni la kiutamaduni tu.
Zipo tabia mbalimbali za Wanaume ambazo hutofautiana kulingana na matukio, lakini zipo zile ambazo ni za kawaida kwa Wanaume wote lakini kwa leo ningependa uzifahamu chache ili kwa Wanawake wasipate shida sana pale wanapokutana na viashiria au tabia halisi za wenza wao.
1. Kukosa uaminifu.
Mwanaume ni mtu wa kupenda kujaribu jaribu na ni vigumu zaidi kwa kiumbe huyu kuacha tabia ya kumiliki Wanawake wengi. Wakati fulani mapenzi huzidi kwako baada ya kujaribu jaribu, hivyo Mwanamke usishtuke ukiona ameongeza mapenzi kwako, ujue alikutana na majanga.
2. Kukosa heshima kwenye fedha.
Wanaume wengi hufikiri wanaweza saidia kila mtu au kufanya kila kitu na tabia hii ndiyo sababu huwafanya wengi wao wafilisike. Mwanaume akipata mke mwenye maamuzi na matumizi sahihi, Pesa ya Mwanaume huongezeka.
3. Kuchelewa kurudi nyumbani.
Asili ya mwanaume ni kijiweni, wacheni wanapochelewa wala msikwazike. Mwanaume hupenda siku yake iishe kwa kuwasiliana na marafiki zake na kupata taarifa mpya za kijiweni ili aweze kuwa sawa.
4. Kuleta wageni nyumbani.
Tena wakati mwingine waandaliwe na chakula, bila kumtaarifu mke, Wanawake wengi hukwazwa na hii tabia na wengi wao huwa hawana la kufanya ni basi tu watafanya nini. Kwa mwanaume kumleta rafiki yake Nyumbani ni kitu kizuri tena hasa akikuamini mkewe.
5. Kukosa hela.
Hii ni tabia ya kawaida sana kwa Mwanaume, yaani Mwanamke ukiingia kwenye ndoa ukakutana nayo tu, usishtuke na wala hutakiwi kushtuka kwani atakosa hela narudia tena atakosa hela kuna siku atakuwa hana, ni tabia ya hovyo lakini uhalisia atakuwa hana.