Vilabu vikubwa vya mpira wa miguu nchini Tanzania, Simba, Yanga na Azam vinatarajiwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Shindano la Kimataifa la kusoma na kuhifadhi Qur’an.
Shindano hilo, linatarajiwa kufanyika Agosti 31, 2024 na Rais Dkt. Samia amepangwa kuwa mgeni rasmi kwenye tukio hilo linalowahusisha wanawake kutoka nchi 12, ikiwemo Tanzania.
Shindano hilo lililoanzishwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania – BAKWATA, linatarajiwa kuanza mapema asubuhi, huku likipanga kumpa tuzo Rais Samia ya kutambua mchango wake wa kuliongoza vema Taifa tangu ashike madaraka ya urais.