Kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa barani Afrika – CDC, kimesema kuna ongezeko kubwa la maambukizi ya ugonjwa wa homa ya nyani.
Mkuu CDC Afrika, Dkt. Jean Kaseya Amesema kwa wiki iliyopita wameorodhesha wagonjwa wapya 4,000 wa homa ya nyani huku ikitoa wito wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo ambazo zilitarajwa kuwasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC.
Amesema, tayari kumeripotiwa vifo vya watu 81 vilivyotokana na ugonjwa huo barani Afrika na kufikisha jumla ya vifo 622 na wagonjwa 22,863 hadi kufikia sasa.
Tayari Umoja wa Ulaya – AU na Marekani zimeahidi kutoa dozi 380,000 za chanjo za ugonjwa huo, ambayo hata hivyo ni ni chini ya asilimia 15 ya dozi ambazo zinazohitajika ili kukabiliana na mlipuko wa homa ya nyani nchini Kongo.