Unapojikuta kwenye treni isiyo sahihi, usisite kushuka kwenye kituo cha kwanza kabisa kwani kadri unavyoendelea kukaa, ndivyo utakavyosogea mbali zaidi kutoka mahali unapokusudia kuwa na safari ya kurudi itakua ngumu na ya gharama kubwa zaidi.

Lakini hii sio tu kuhusu treni, bali inahusu pia inahusu maisha, kwakuwa unapoelekea kwenye njia mbaya iwe katika uhusiano, kazi, au chaguo ambalo umefanya itambue mapema na uwe na ujasiri wa kuondoka, kiufupi fanya mamuzi ya mapema kwa kila jambo na tanguliza umakini.

Unapogeuka haraka, ndivyo itakavyokuwa rahisi kutafuta njia ya kurudi mahali unapotaka kuwa kweli sababu katika maisha kuna mambo mengi tunayakosea ambayo laiti tungetambua mapema au kuchukua maamuzi mapema basi tungefanikiwa kuepuka matatizo zaidi lakini tukipata na funzo.

Hata hivyo binadamu tuna matatizo maana huwa hatukubali ushauri au kujishughulisha kutafuta ukweli wa mambo na wakati mwingine tumekuwa tukidharau mambo au kuwadharau watu na kujiona tumemaliza kila kitu maishani. Hivyo hapa nakupa mbinu zitakazokufanya utambue siri ya maisha na hata ukajiheshimu na kuwaheshimu wengine.

1. Kutembelea Chumba cha Maiti, kutakufanya utambue thamani ya maisha.
2. Kutembelea Hospitali kutakufanya uthamini afya yako na thamani ya utu.
3. Kutembelea Gereza kutakufanya uthamini uhuru ulionao.
4. Mambo unayofurahia na kuyachukulia ni ya kawaida, wengine hawana na wanayahitaji hivyo jikubali jinsi ulivyo.
5. Kila siku kila saa mshukuru MUNGU kwa mambo mazuri aliyokutendea.

Serikali, Kampuni za Nishati wajadiliana uchakataji LNG
Hitilafu ya Umeme yaathiri huduma ya Maji Dsm, Pwani