Israel imekubali sitisho la mapigano kwa saa tisa kila siku katika muda wote wa kampeni ya kutoa chanjo dhidi ya polio katika Ukanda wa Gaza, ambako kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kiligunduliwa mwezi huu wa Agosti.
Kwa mujihu wa Afisa wa Shirika la afya Duniani – WHO, wa ukanda wa Gaza Rik Peeperkorn amesema kampeni hiyo itaanza hapo kesho kutwa Septemba 1, 2024 katikati maeneo ya Gaza kwa siku tatu.
Amesema, “mapigano yatasitishwa wakati wa zoezi la kutoa chanjo kwa siku tatu na timu zetu zitafanya tathmini baada ya siku tatu za kwanza au mbili zaidi ni muhimu, ili watoto wengi wapewe chanjo hiyo muhimu.”
Zoezi hilo, baadaye litahamia kusini mwa Gaza na kaskazini mwa Gaza, likitazamiwa kuchukua siku tatu hadi tano ambapo zaidi ya dozi milioni 1.2 za chanjo ya polio zimekwisha tolewa huko Gaza na 400,000 za ziada zikitarajiwa.