Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya Afya, Dkt. Ntuli kapologwe amesema Serikali inazidi kuchukua tahadhari kubwa ya kujilinda dhidi ya ugonjwa wa mlipuko wa Mpox ambayo unasababishwa na kirusi cha Monkeypox.
Dkt. Ntumi ameyasema hayo katika Mkutano wa Nane wa Tathimini ya Mkataba wa lishe na Kutambulisha Mpango wa Taifa wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto (TMCHIP) uliofanyika leo Jijini Dodoma.
Amesema, Wagonjwa 102,997 wamethibitika kuwa na Ugonjwa huo, huku watu 223 (CFR 0.2%) wakipoteza Maisha Duniani kote ambapo nchi jirani na Tanzania; Kenya, Uganda, DRC, Rwanda, Msumbiji na Burundi tayari zimeripotiwa kuathirika na ugonjwa huo huku Tanzania kukiwa hakuna aliyeripotiwa kuathirika.
Dkt. Ntumi ameongeza kuwa, miongoni wa mikakati iliyochukuliwa ni pamoja na Mafunzo elekezi kutolewa kwa Watumshi 1,671, kutambua wagonjwa, tiba, IPC, Uchunguzi wa Wasafiri, upimaji wa sampuli na Uchunguzi wa wasafiri mipakani unaendelea. Hadi 28 Agosti 2024 wasafiri 139,903 wamechunguzwa na Elimu kupitia vyombo vya habari inaendelea kutolewa.
Aidha, amewataka Waganga wakuu wa Mikoa (RMO) na Halmashauri (DMO) kuendelea kutekeleza Sheria ya Afya ya Jamii na Kanuni za Afya za Kimataifa ambazo zinataka Kutoa taarifa kwa njia ya haraka kwa Mganga Mkuu wa Serikali ndani ya saa 6 tangu kupata taarifa husika.
Hata hivyo amesema Waganga Wakuu wanapaswa kuchukua hatua stahiki za kuzuia kusambaa kwa ugonjwa na kudhibiti tukio husika, Kutekeleza hatua za makatazo mbalimbali ya udhibiti ikiwemo kuweka karantini pale inapohitajika.