Ghana imefuata hatua za Nigeria na Côte d’Ivoire, za kusitisha mauzo yake ya nafaka bada ya Waziri wa Kilimo wa Taifa hilo, Bryan Acheampong kudai kumekuwepo na ukame mkali ambao umeathiri uzalishaji unaotishia suala la uhaba wa chakula.
Acheampong amesema maeneo sita ya kaskazini na mashariki mwa Taifa hilo yanatoa takriban asilimia 62 ya nafaka ambayo yote yameathiriwa na ukame.
Amesema, hali ambayo imekuwa ikiendelea kwa miezi miwili na ambayo tayari imesababisha hasara kwa wakulima karibu nusu milioni, huku kukiripotiwa uhaba wa mchele, mahindi na soya.
Wakati huo huo, Waziri wa Fedha wa Ghana, Mohammed Amin Adam amesema Ghana itatumia hifadhi ya nafaka ya ECOWAS na kushirikiana na sekta ya kibinafsi kuagiza nafaka zilizokosekana.