Rais wa Kenya, William Ruto amesema atarejea katika uinjilisti baada ya kustaafu kwani ndio ulikuwa wito wake wa kwanza kabla ya kujitosa katika siasa.

Ruto ameyasema hayo Septemba 1, 2024 alipohudhuria ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kianglikana la ACK, Cathedral lililopo mjini Bungoma.

Amesema, “mimi ni mwinjilisti na nyakati zingine watu hushangaa kwa nini mimi husimama kwenye majukwaa hata juu ya magari. Ikiwa wewe ni mwinjilisti, nyakati nyingi huwa unadhihirisha tabia za mwinjilisti hata unapofanya mambo mengine,” Rais Ruto akasema.”

William Ruto na Mkewe wakitoka Kanisani.

Ruto ameongeza kuwa, mwenendo wake wa kuwahutubia waumini katika madhabahu na maeneo ya wazi unatokana na mafundisho yake ya uinjilisti ambayo yamemkuza tangu utotoni.

“Nimeamua kwamba nikistaafu kama Rais nitarejelea kazi ya uinjilisti kwa sababu hiyo ndio mwito wangu asilia, pia ninawataka viongozi wa makanisa kuendelea kuliombea taifa ninapoendelea kung’ang’ana kukarabati uchumi wa Kenya,” alisema Ruto.

Mpunga arejeshwa Dodoma jiji
Waganga wamkana aliyekamatwa na Mafuvu 24 ya binadamu