Naibu katibu Mkuu Ofis ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya, Dkt. Grace Magembe amewataka watoa huduma katika Sekta ya afya kuzingatia ubora na ufanisi katika kutoa huduma hizo kwa wananchi ili waweze kuona faida za uwekezaji katika afya ambao umefanywa na Serikali.

Dkt. Grace ameyasema hayo mapema leo katika kikao kazi cha Tathimini ya Huduma za Chanjo katika Mikoa na Halmashauri kwa kipindi cha January – Juni 2024 ambao kimehudhuriwa na Waganga wakuu wa Mikoa na Waratibu wa Chanjo wa Mikoa kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel Mkoani Dodoma.

Amesema, Serikali imejitahidi sana kuweka miundombinu bora ya afya hivyo watendaji wa sekta ya afya wanatakiwa kuzingatia ubora na ufanisi hasa katika utoaji wa huduma za afya Msingi kwani huko ndiko Wananchi wengi ndipo wanapokwenda kupata huduma.

Dkt. Grace amewataka watendaji hao kuongeza ubunifu katika utendaji kazi wao ili kuendelea kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Wananchi.

“Kama unafikiri kuna namna nzuri ya kufanya jambo flani ili kuboresha utoaji wa huduma usikae nalo liwasilishe kwa sababu nyinyi ndo mpo katika maeneo ya utendaji na mnaona namna huduma zinavyotolewa nasi ofisi ya Rais TAMISEMI tutalipokea na kulifanyia kazi,”  alisema.

Aidha amewataka watumishi wa sekta ya afya kufanya kazi kwa Pamoja na kushirikiana (intergration approach) kwani sekta ya afya huduma zake zinaingiliana katika kuboresha afya za wananchi.

Mkutano FOCAC: Rais Samia awasili China
Tanzania ipo tayari kujifunza - Rais Dkt. Mwinyi