Mshambuliaji kiongozi wa Bayern Munich ,Harry Kane ameendelea kufanya vyema kwa kuweka rekodi mbalimbali tangu ajiunge na klabu hiyo mwezi Agosti 2023.Nyota huyo amekuwa na mwendelezo mzuri tangu ajiunge na the bavarians akifunga jumla ya mabao 46 kwenye michezo 48 aliyocheza .

mbali na kushindwa kuipa Bayern munich taji la Bundesliga na UEFA Champions League nyota huyo aliweza kutwaa tuzo binafsi za mfungaji bora wa Bundesliga kwa mabao 36 katika mechi 32 alizocheza na Mfungaji bora UEFA champions League kwa mabao 8 katika mechi 12. Kane hakuishia tu kuwa mfungaji bora wa klabu hiyo bali aliibuka mfungaji bora wa michuano ya EURO 2024 iliyofanyika nchini Ujerumani akifunga mabao 3 sawa na Cody Gakpo,Mikauta ,Musiala,Ivan Schranz na Dani Olmo.

Kane alisaini mkataba wa muda mrefu wa kuitumikia Bayern Munich na atakuwepo klabuni hapo mpaka mwaka 2027 . Malengo makubwa ya klabu hiyo ni kutwaa ubingwa wa UEFA,Kombe la Dunia la vilabu kwa mwaka 2025 na kurejesha kombe la Bundesliga walilopoteza msimu wa 203/24 .

Msimu wa 2024/25 Kane amecheza michezo 2 akifunga bao 1 na kutoa pasi za mabao 2.Kazi pekee aliyonayo kwa sasa ni kuvunja rekodi ya Robert Lewandowski aliyefunga mabao 344 katika mechi 375 na kutoa asist 73. Lewandowski aliweza kutwaaa makombe ya Bundesliga mara 9 kombe la dunia kwa vilabu mara 1 ,UEFA 1 na aliweza kuvunja rekodiĀ  mbali mbali za Gerd Muller.

Baada ya Mbappe kuikacha PSG nyota mwingine atimkia Saudi Arabia
Ukandamizaji chanzo cha migogoro, vita barani Afrika