Johansen Buberwa – Kagera.

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa, Zaituni Msofe amewataka Madiwani kwa kushirikiana na Serikali katika kuchukua tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Mpox katika maeneo yao.

Ameyasema hayo katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, wakati akitoa salamu za Serikali katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika wakati wa kujadili taarifa utekelezaj robo ya nne  ya mwaka wa fedha Aprili hadi Juni 2023/2024.

Msofe amesema Serikali kupitia Idara ya Afya inatakiwa kuendelea kuweka mikakati mbalimba ya kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu tahadhari na namna ya kujikinga na ugonjwa huo.

Amesema licha ya kwamba ugonjwa huo haujatangazwa kuingia nchini Tanzani lakini ni vizuri wananchi kupatiwa elimu namna bora ya kujilinda kuhusu ugonjwa huo na kuanza kuchukua tahadhari mapema.

Dkt. Ndumbaro amuongezea adhabu aliyekiuka maadili
Fedha za Mazingira zainufaisha Zanzibar