Uzoefu katika masuala ya Polisi Jamii umetolewa ufafanuzi katika mafunzo kwa Askari wa kike na wasimamizi wa sheria duniani yanayoendelea jijini Chicago Nchini Marekani na Kamishna wa Polisi Utawala na Menejimenti ya Rasilimali Watu, CP Suzan Kaganda katika maeneo aliyohudumu akiwa Mkuu wa Operesheni Abyei, Sudan kusini.

CP Kaganda ametoa uzoefu huo Nchini humo mbele ya maelefu ya waliohudhuria mafunzo hayo yaliyohusisha Nchi zaidi ya 64 na kusema Wananchi wanaweza kushiriki kulinda amani ya eneo husika bila ya kuwa na Jeshi la Polisi wala Jeshi lolote, katika eneo lenye changamoto ya amani.

Amesema, amani ni jambo ambalo linatakiwa kushirikisha Jamii ili amani na utulivu wa eneo husika uimarike kutokana na ushiriki kamili wa Wananchi katika ulinzi wa amani kwa kuhusisha Jamii husika na kusisitiza kuwa Polisi jamii ni njia nzuri katika ulinzi wa amani kutoka na tafiti alizozifanya na uzoefu wake.

Aidha, washiriki wengine kutoka Tanzania wakaeleza namna mafunzo hayo yalivyowaimarisha katika kujiamini kiutendaji na nafasi wanazopewa hudumu, huku wakiweka wazi kuwa pindi watakaporejea nyumbani Watanzania wategemee mabadiliko kutokana mafunzo hayo.

Naye Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi, SACP Johari Saidi amesema mafunzo hayo yamewapa mwanga katika mgawanyo wa majukumu bila kuathiri familia walizonazo, ikiwa ni pamoja na namna bora ya utunzaji wa afya kwa Askari kutokana na unyeti wa majukumu waliyonayo.

Kampeni ya Nishati Safi ya kupikia yaendelea kuungwa mkono
Ujerumani yamtambulisha nahodha mpya mrithi wa Gundogan