Joshua Kimmich ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa Ujerumani kufuatia Ilkay Gundogan kustaafu kimataifa mwezi uliopita.Mchezaji huyo wa Bayern Munich ameichezea timu ya taifa mara 91 tangu alipocheza kwa mara ya kwanza Mei 2016, akifunga mabao sita, na amekuwa nahodha wa kikosi hicho mara 17 zilizopita.

Kimmich alicheza katika mechi zote tano za Ujerumani kwenye Euro 2024 walipofika robo-fainali, huku Nagelsmann akithibitisha jinsi mchezaji huyo mwenye uwezo mwingi.

Antonio Rudiger wa Real Madrid na Kai Havertz wa Arsenal, ambaye alikuwa nahodha wa Ujerumani katika ngazi ya vijana, wamechaguliwa kuwa makamu wa nahodha . Kocha  Julian Nagelsmann amenukuliwa akisema

“Nahodha anaweka maoni ya timu . Kimmich alikuwa mrithi wa kimantiki,Anaongoza njia kwa mawazo yake. Tuna mchanganyiko mzuri sana na wachezaji hawa watatu.”

Marc-Andre ter Stegen, Jonathan Tah, Niclas Fullkrug na Pascal Gross pia wamechaguliwa kwa baraza jipya la uongozi la Ujerumani.

“Baraza la timu ni kundi zuri sana, linalowajibika,Tuliichagua vyema; wachezaji wote walikuwa na furaha na wana nia ya kutimiza majukumu yao.” aliongeza Nagelsmann

CP Kaganda atoa uzoefu masuala ya Polisi Jamii
Ronaldo afunguka hatma yake kwa timu ya Taifa