Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Rashid Mfaume amewataka watumishi wa afya kuongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi kuanzia ngazi ya chini ya kituo cha afya hadi ngazi ya juu ili kuendelea kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Dkt. Mfaume amesema hayo wakati akifunga kikao kazi kwaniaba ya Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia afya, Dkt. Grace Magembe cha Tathimini ya Huduma za Chanjo katika Mikoa na Halmashauri kwa kipindi cha Januari – Juni 2024.
Kikao kazi hicho, kilichofanyika kwa siku mbili kilihudhuliwa na Waganga Wakuu wa Mikoa Pamoja na Waratibu wa chanjo wa Mikoa kilichofanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel Mkoani Dodoma.
“Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amekuwa akisisitiza uwajibikaji wa kila mmoja wetu kwa nafasi yake, hivyo wewe kama kiongozi unapaswa kuwajibika kwa kuwasimamia watendaji katika mkoa wako,” amesema Dkt. Mfaume.
Hata hivyo, amesema kuna maeneo ambayo wamekuwa wakifanya vizuri yafaa kuyaendeleza nakuboresha zaidi kwani kwasasa kuna vitendea vya kutosha katika uwezeshaji wa huduma za afya.