Afisa Tarafa Mpapura, Emmanuel Shilatu aliwatembelea, kuwapa pole na faraja wakazi wa Kijiji cha Mpapura baada ya kupatwa na janga la moto kuunguza nyumba 2, jiko Moja.
Kwenye tukio hilo, Maimuna na majirani zake wakazi wa Kijiji cha Mpapura Kata ya Mpapura nyumba zao zimeungua moto hapo jana Septemba 3, 2024.
Moto huo ulisababishwa na Watoto kuwasha moto kwenye Moja wapo ya nyumba wakati wakicheza.