Katika kuhakikisha Askari Wanawake wanakuwa imara na mahiri katika kila nyanja wanazohudumu, wamejengewa umahiri katika ulengaji wa Shabaha na wabobezi (Sniper) kutoka Jeshi la Polisi Nchini Marekani.

Miongoni mwa Askari hao waliopata mafunzo hayo ni Koplo wa Jeshi la Polisi Kutoka Nchini Tanzania, CPL Salome Masanyiwa ambaye amebainisha kuwa yamemjenga na kumuongezea umahiri tofauti na kipindi cha Nyuma.

Amesisitiza kuwa anakwenda kupeleka ujuzi huo alioupata kwa Askari wengine wa  Tanzania ambao hawakupata fursa ya mafunzo hayo.

Serikali yapanga kuzitengea fedha barabara korofi
Majaliwa: Tanzania itaendelea kujiimarisha Kidiplomasia