Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa barani Afrika – CDC, kimesema shehena ya kwanza ya dozi 100,000 za chanjo ya mpox itawasili nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC, hii leo Septemba 5, 2024 huku chanjo zingine 200,000 zikitarajiwa.
CDC imesema chanjo hizo za ziada zitawasili wiki hii katika Nchi hiyo kubwa ya ukanda wa Afrika ya Kati yenye watu milioni 100 ambayo ni kitovu cha mlipuko wa mpox, iliyoripotiwa kuwa visa vingi na vifo vinavyozidi kuongezeka.
Mkuu wa kituo cha Afrika cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, Jean Kaseyaa amesrma zaidi ya dozi 99,000 zinatarajiwa kuwasili hii leo Alhamisi Septemba 5, 2024.
Kwa mujibu wa taarifa za Shirika la Afya Duniani – WHO, zinaeleza kuwa zaidi ya visa 17,500 na vifo 629 vimeripotiwa nchini DRC tangu mwanzoni mwa mwaka 2024.