Chama cha soka nchini Ufaransa kimetangaza walioteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d’Or 2024 . Majina ya wachezaji wanaowania tuzo hizo yameangazia zaidi wachezaji kutoka Real Madrid (washindi wa Ligi ya Mabingwa), Timu ya Taifa ya Uhispania (mabingwa wa Euro 2024), na Timu ya Kitaifa ya Argentina (mabingwa wa Copa América).
Miongoni mwa majina makubwa yaliyotangazwa ni Erling Haaland, Martin Ödegaard, Declan Rice, Vitinha, Harry Kane, Federico Valverde, na Antonio Rüdiger.
Wachezaji sita wa kikosi cha timu ya taifa hispania wako katika kinyang’anyiro cha kuwania Ballon d’Or mwaka huu baada ya ushindi wao wa Euro 2024.Nico Williams, Dani Olmo, Rodri, Dani Carvajal, Lamine Yamal, na Alejandro Grimaldo.
Wachezaji wa wawili pekee kutoka timu ya taifa ya Argentina walioshinda ubingwa wa Copa América ndio wanawakilisha bara la Amerika Kusini ambao ni kipa Emiliano Martínez na fowadi Lautaro Martínez.
Kwa mara ya kwanza tangu 2003, si Cristiano Ronaldo wala Lionel Messi kati ya walioteuliwa. Mchezaji wa Barcelona Lamine Yamal, ambaye alitimiza umri wa miaka 17 mwezi Julai, anakuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuteuliwa kuwania tuzo ya Ballon d’Or.
Yamal pia yuko katika kinyang’anyiro cha Kombe la Kopa, linalotunukiwa mchezaji bora chipukizi, pamoja na vipaji kama Pau Cubarsí (Barcelona) na Arda Guler (Real Madrid).
Kipengele cha makocha, mameneja wa hispania wanatawala kipengele hicho kikiwa na Xabi Alonso, Pep Guardiola, na kocha wa timu ya taifa ya Uhispania, Luis de la Fuente. Watashindana na Waitaliano Carlo Ancelotti (Real Madrid), Gian Piero Gasperini (Atalanta), na kocha wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Scaloni. Sherehe ya tuzo hizo itafanyika mjini Paris mnamo Oktoba 28.