Mwanasiasa wa upinzani wa Chama cha National Unity Platform – NUP nchini Uganda, Bobi Wine anatarajiwa kufanyiwa upasuaji baada ya kujeruhiwa na Polisi kwa risasi mguuni.

Awali chama chake kilikuwa kimeripoti kwamba kiongozi huyo wa upinzani alipigiwa risasi kwenye mguu wake wakati wa mvutano kati yake na maofosa wa polisi.

Bobi Wine ambaye ni mkosoaji mkubwa wa rais wa Uganda, Yoweri Museveni na alikumbwa na shambuli hilo wakati akiwa mji wa Bulindo uliopo kilomita 20 kutoka jiji kuu la Kampala, wakati NUP iliporipoti kutokea kwa tukio hilo.

Wakili wa mwanasiasa huyo, George Musisi, amesema Bob Wine anaendelea vizuri lakini Madaktari wake wanahitaji kumfanyiwa upasuaji ili kuondoa vipande vya chuma huku akidai Polisi walimlenga kimakusudi mwanasiasa huyo wa upinzani.

Amesema, alipigwa risasi hiyo baada ya maofisa wa Polisi kuanza kurusha mabomu ya machozi kuelekea eneo ambapo alikuwa akikutana na wafuasi wake katika mjini Bulindo na tayari wamesema watafanya uchunguzi juu ya tukio husika.

Moloko afunguka ilipofeli Stars dhidi ya Ethiopia
Manchester City na Arsenal watikisa tuzo za Ballon D'OR