Taifa stars imeanza kwa sare ya bila kufungana na Ethiopia mchezo wa kwanza wa kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) na Mchezo huo ulipigwa dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam. Matokeo hayo ya Stars si mazuri sana kwa nyumbani kwani itatakiwa kucheza kwa ustadi mkubwa mechi zinazofuata dhidi ya Guinea na DRC Congo.

Kikosi cha Stars kilikuwa na mabadiliko makubwa ya wachezaji na wengi wakiwa vijana wenye uwezo mkubwa.Uwezo mkubwa wa mchezaji mmoja mmoja uliifanya Stars Kucheza kwa weledi mkubwa katika mechi hiyo. kocha Hemedi Suleiman alianza na kikosi kilichoundwa na Ally Salim,Lusajo Mwaikenda ,Mohammed Hussein ,Ibrahim Abdulla,Dickson Job,Himid Mao ,Edwin Balua,Novatus Dismas ,Feisal SALUM,Clement Mzize na Nickson Kibabage.

Matokeo hayo ya sare yanaifanya Stars kukosa kiasi cha Sh.Milioni 20 ahadi kutoka kwa vilabu vya Simba,Yanga na Azam kama wangefunga mabao kuanzia matatu. lakini pia  Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 5 kwa kila bao kama wangeshinda mchezo huo.

kocha Mkuu Hemed Suleiman amenukuliwa akisema

” kama hatujafunga inamaanisha kuwa tunachangamoto ya kuingiza mpira kwenye wavu, Tulitengeneza nafasi lakini hatujafunga na hapa tunarudi katika uwanja wa mazoezi na kufanya maboresho. Hatuwezi kila siku tukawa tunapata sare. Tumemaliza mechi salama na ilikuwa ni mechi ngumu tumeanza slow na tulikuwa tunaprogress baada ya muda mpaka kipindi cha pili.Tumetengeneza nafasi zaidi dakika 20 za mwisho za kipindi cha pili lakini hatukufanikiwa kuzitumia.Tunarudi katika uwanja wa mazoezi kuangalia mapungufu na tutayafanyia kazi”

”Hii timu inafanya transition na ukiangalia wachezaji wetu ni wadogo na wanahitaji muda ,sasa hivi tunatakiwa kuwapa zaidi moyo wa kupambana .Ninaamini watafanya vizuri muda mfupi ujao”

 

Jifunze kwa Tai: Jambo jema haliji kirahisi
Shambulio la risasi: Bob Wine kufanyiwa upasuaji