Vijana wahitimu wa mafunzo ya kwa mujibu wa sheria oparesheni miaka 60 ya Muungano ya kikosi namba 832 KJ Ruvu, wameahidi kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kujenga uchumi imara kwa maslahi ya taifa kutokana na mafunzo ya jeshi la awali waliyopata.

Akisoma risala kwa niaba ya Wahitimu huko Ruvu Kibaha mkoani Pwani. Hilda Edward amesema kutokana na mafunzo ya wiki 12 waliyopata wameweza kujifunza utii, Uzalendo, uadilifu na kuchapa kazi na kuahidi kuzingatia mafunzo yote kwa kuhakikisha rasimali za nchi yetu hazipotei wakizingatia mafunzo waliyopatiwa katika kipindi chao cha mafunzo.

Amesema, “tunaahidi kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt Samia Suluhu Hassan katika kujenga uchumi imara kwa maslahi mapana ya nchi yetukudumisha uzalendo, utii nidhamu uaminifu na kwa Taifa.

Aidha, Wahitimu hao kwa pamoja wamekula kiapo cha utii kwa amiri jeshi Mkuu na kutoa shukrani za pekee kwa Wakufunzi wao kwa kuwapatia stadi za maisha katika kipindi chote cha miezi mitatu walipokuwa kikosini hapo wakijifunza ukakamavu, kilimo na ufugaji, usanii na michezo.

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amewataka wahitimu hao kwenda kutumia mafunzo waliyoyapata kujipatia fursa na kuwa mabalozi wema kwa vijana wengine.

Mwakilishi wa Mkuu wa Majeshi, Brigedia Jenerali Solitina Bernad Nshushi amewapongeza kwa kujifunza mafunzo haya ya kwa mujibu wa sheria kwa sababu kwa kufanya hivyo wamejitende haki wenye na katika jamii waliyotoka na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa JKT, Kanali George Barongo amesema haya mliyoyapata sasa mmefahamu dhana ya uzalendo mmekua tayari kutumikia taifa popote mtakapokuwa hivyo basi mnapaswa mkatumie elimu hiyo pasipokuvunja utaratibu na sheria za nchi.

Naye Kamanda Kikosi cha Ruvu JKT, Kanali Peter Elias Mnyani amesema vijana waliohitimu mafunzo yao wamejifunza stadi za maisha elimu hii waliyoipata imewajenga kifikra mbalimbali za ulinzi na usalama na wamekidhi vigezo.

Watakiwa kuendana na kasi mabadiliko ya Kiteknolojia
Machali ataka wananchi wapewe elimu tahadhari ya Mpox