Afisa mtendaji mkuu wa Wakala wa usajili wa Biashara na leseni nchini ( BRELA) Godfrey Nyaisa ameongoza ufunguzi wa kikao cha kimataifa cha mashauriano na wadau kuhusu Mkatabata wa Sheria ya kimataifa ya shirika la miliki ubunifu Duniani (WIPO) ya ulinzi wa maumbo na michoro bunifu kilichofanyika mapema leo 05 septemba 2024

Nyaisa amesema kuwa eneo la miliki bunifu nchini ni moja ya nchi wanachama wa shirika la miliki ubunifu la kanda ya Afrika ( AFRICAN REGIONAL INTELLECTUAL PROPERTY ORGANIZATION—ARIPO).

Amesema, “kupitia mashirika haya nchi yetu imesaini na kuridhia mikataba na itifaki mbalimbali zinazohusu usimamizi na uratibu wa miliki ubunifu kikanda na kimataifa ambapo mikataba na itifaki hizi zimeweka mifumo inayowezesha usajili na ulinzi wa nyenzo za miliki ubunifu katukangazi ya kikanda na kimataifa, hivyo kuongeza wigo wa usajili na ulinzi wa nyenzo hizo kwa nchi wanachama.”

Nchi wanachama za WIPO zimeendeleea kuandaa mikakati na njia za kuhakikisha miliki ubunifu inatumika kama chachu ya maendeleo duniani na ,mnamo mwezi julai 2022 WIPO iliridhiwa kuandaliwa kwa mkutano wa kidiplomasia wa kukamilisha na kupitishwa kwa mkataba wa sharia hiyo.

Aidha mkutano wa kidiplomasia utakaokamilisha na kuridhia mkataba huo baada ya kupitishwa na nchi wanachama umepangwa kufanyika kuanzia Novemba 11-22, 2024, huku akifafanua kwamba mkataba huo unalenga kuweka utaratibu au mfumo wa kimataifa wa usajili na ulinzi wa maumbo bunifu kwa nchi na mashirika wanachama wa WIPO.

Nyaisa amefafanua Zaidi na kusema kwamba mfumo huu utaongeza wigo wa ulinzi katika nchi nyingi kwa mara moja badala ya nchi moja kwa moja ambazo mbunifu anahitajika kulinda ubunifu husika hivyo kupunguza gharama na ugumu wa ulinzi wa ubunifu.

Brela ambayo pia ni ofisi ya taifa ya miliki ubunifu chini ya wizara ya viwanda na biashara ambayo ndio wizara inayoratibumiliki ubunifuhapa nchini imeandaa kikao hiki muhimu leo ikiwa ni kuhjadili na kutoa maoni juu ya mkataba huo wa kimataifa ikiwa ni maandalizi ya uidhinishwaji katika mkutano wa kidiplomasia uliotajwa hapo juu.

Afisa mtendaji huyo ameongeza kuwa endapo sheria hii itapitishwa na baadae Tanzania kuiridhia itatoa fursa na kuongeza wigo kwa wabunifu wa maumbo / michoro bunifu kusajili na kulinda maumbo na michoro bunifu yao katika ngazi ya kimataifa hivyo kukuza biashara na kuwawezesha kuhimili ushindani katika masoko ya ndani na nje.

Pia kikao hiki kimehudhuriwa na wadau kutoka maeneo mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mustafa A Haji Assistant Registrar of IP, Zanzibar Business and Property Registration Agency ( BIRA), Dkt. Perfect Melkioni na wadau wengine.

 

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 6, 2024
Watakiwa kuendana na kasi mabadiliko ya Kiteknolojia