Takriban Wanafunzi 17 wamefariki kwa ajali ya Moto na wengine 13 kujeruhiwa vibaya katika Shule ya Msingi ya Hillside Endarasha iliyopo Kaunti ya Nyeri nchini Kenya.

Akiongea hii leo Septemba 6, 2024, Msemaji wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi, Resila Onyango amesema wanafunzi 14 walipelekwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya kufuatia moto huo uliotokea usiku wa Septemba 5, 2024.

“Chanzo cha moto huo uliotokea Alhamisi usiku katika Shule ya Msingi ya Hillside Endarasha kaunti ya Nyeri kinachunguzwa, tunachunguza sababu na tutachukua hatua zinazohitajika.”

Ajali za Moto katika mabweni ya shule nchini Kenya imekuwa ni jambo la kawaida, ambapo Wanafunzi wengi hukaa huko kwasababu wazazi huamini kuwa inawapa muda zaidi wa kujisomea.

Itakumbukwa kuwa Mwaka 2017, Wanafunzi 10 wa shule ya upili walikufa kwa moto katika shule moja jijini, Nairobi.

Mbeya: Ajali ya Basi yauwa 12, majeruhi 36
Tetesi za usajili Duniani leo 06 septemba 2024