Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufunga bao la 900 katika maisha yake ya soka.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 alifunga bao hilo katika mchezo wao wa Ligi ya Mataifa dhidi ya Croatia, na kuwapa Ureno  ushindi wa mabao 2-1.

Bao hilo lilikuwa la 131 kwake kwa nchi yake, huku akiwa amefunga pia katika ngazi ya vilabu kama Sporting Lisbon, Manchester United, Real Madrid, Juventus na Al-Nassr.

Mwanzo mzuri kwa Ronaldo

Alifunga mabao mawili kwa Sporting ya Ureno tarehe 7 Oktoba 2002, akiwa na umri wa miaka 17 miezi minane na siku tatu katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Moreirense.

Kisha akahamia Manchester United, akifunga mabao 118 katika mechi 293 akiwa na Mashetani Wekundu kabla ya kujiunga na Real Madrid mwaka 2009 kwa rekodi ya dunia ya euro 94m (£80m).

Kwa miaka tisa akiwa na wababe hao wa Uhispania alifunga mabao 450 katika mechi 438 pekee kabla ya kwenda Italia kujiunga na Juventus.

Aliongeza mabao mengine 101 kwenye jumla ya mabao yake katika kipindi cha miaka mitatu akiwa na klabu hiyo ya Italia kabla ya kurejea United, ambapo angefunga mabao 27 katika michezo 54.amnamo 2023 alihamia Saudi Arabia na kujiunga na Al-Nassr ambapo amefunga mabao 68 na kuhesabu.

REKODI YA MABAO YA RONALDO

TIMU ALIZOCHEZEA MABAO ALIYOFUNGA
Al-Nassr 68
Juventus 101
Manchester United 145
Portugal 131
Real Madrid 450
Sporting CP 5
JUMLA: 900

Je Ronaldo ni zaidi ya Pele na Romario?

Hakuna data kamili inayoonyeshamfungaji bora wa muda wote wa soka la wanaume, lakini Ronaldo alikuwa tayari anaongoza kwa michezo rasmi, akiwa amevuka mabao 800 katika kipindi chake cha pili akiwa Manchester United.

Gwiji wa Brazil Pele na Romario walidai tofauti kuwa wamefunga zaidi ya mabao 1,000 kila mmoja, lakini wakachuja mechi za kirafiki na nambari hizo kushuka hadi mabao 700.Wataalamu wa takwimu wasio rasmi RSSSF, wa nje wanasema Pele alifunga mabao 778, huku Romario akifunga 785.

Lionel Messi, mpinzani wa muda mrefu wa Ronaldo, amefunga mabao 867 hadi sasa.

Ronaldo ataka bao la 1000

Muda hauko upande wa Ronaldo kwani sasa ana umri wa miaka 39, lakini mkongwe huyo amedhamiria kuendelea kucheza hadi afikishe idadi ya mabao 1,000 katika maisha yake ya soka.

Akiongea na mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand katika mahojiano kwenye chaneli yake ya YouTube, Ronaldo wa nje alisema ana imani kwamba anaweza kupiga hatua hiyo ndani ya miaka michache ijayo.

“Nataka kufikisha mabao 1,000,Ikiwa sina majeraha yoyote, hili kwangu ndilo jambo muhimu zaidi, nataka hilo.Mabao yote niliyofunga, yana video.”

Tetesi za usajili Duniani leo 06 septemba 2024
Hispania yatikisa tuzo za Ballon D'or