Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameiagiza Wizara ya Kilimo isimamie kwa ukaribu upatikanaji na usambazi wa pembejeo za kilimo hususani mbolea ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa kilimo na kwa kuzingatia jiografia za kanda za kilimo nchini.

Majaliwa ameyasema hayo leo hii leo Septemba 6, 2024 wakati wa kuahirisha Mkutano wa 16 wa Bunge, jijini Dodoma na kuwataka pia Maafisa Ugani waendelee kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi ya teknolojia bora za uhifadhi wa mazao ya chakula na matumizi sahihi ya chakula hicho katika ngazi ya familia.

Mbowe ataka fidia ya Bilioni 5 kwa Msigwa
Majaliwa atoa maelekezo uendeshaji Mradi SGR