Polisi waanza uchunguzi vifo Wanafunzi 17 Shuleni

Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Nchini Kenya, Gilbert Masengeli amesema Polisi wameanzisha uchunguzi ili kubaini chanzo vifo vya Wanafunzi 17 waliofariki kwenye ajali ya moto katika shule ya Hillside Endarasha Academy Kieni iliyopo Kaunti ya Nyeri.

Akiongea mjini Mombasa, Masengeli amesema idara zinazohusika katika kufanya uchunguzi wa mikasa pamoja na jinai wamefika eneo la tukio kutathmini hali halisi.

Mapema hii leo Septemba 6, 2024, Msemaji wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi, Resila Onyango amesema wanafunzi 14 walipelekwa hospitalini wakiwa na majeraha mabaya kufuatia moto huo uliotokea usiku wa Septemba 5, 2024.

Ajali za Moto katika mabweni ya shule nchini Kenya imekuwa ni jambo la kawaida, ambapo Wanafunzi wengi hukaa huko kwasababu wazazi huamini kuwa inawapa muda zaidi wa kujisomea.

Itakumbukwa kuwa Mwaka 2017, Wanafunzi 10 wa shule ya upili walikufa kwa moto katika shule moja jijini, Nairobi.

Ni wakati wa Kibwana Shomari kuondoka Yanga
Sureboy awekwa kikaangoni Yanga