Johansen Buberwa – Kagera.

Kesi  ya mauaji ya Jamhuri namba 17740 ya mwaka 2024  ya mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath inayowakabili washitakiwa tisa akiwemo Padri Elipidius Rwegoshora na wenzake nane imetajwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya Bukoba Mkoani Kagera ambapo vielelezo 37 na maelezo ya mashahidi 52 ambayo vimetumika.

Maelezo ya mashahidi hao 52 yamesomwa  mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Elipokea Yona na mwendesha mashitaka  wa mkoa wa kagera  Waziri Magumbo pamoja na mawakili wengine wa serikali ambao ni Nassoro Katuga, Sabina Silayo, Erick Mabagala pamoja na Matrida Assey.

Maelezo mengine ya mashahidi 52 yaliyotolewa mahakamani hapo ni kwamba mshitakiwa namba moja padri Elipidius Rwegoshora wakati  anamushawishi Baba Asimwe pamoja na washitakiwa wengine kufanya kitendo hicho  cha kupata viungo vya mtoto huyo aliwaambia kuwa awatakiwi kumwambia mtu yeyote yule  kwani yeye tayari ashaenda kwa mgaga wa kienyeji na  wakimwambia mtu mwingine hilo dili watakufa.

Maelezo mengine ni kuwa washitakiwa baada ya kufanikiwa kumteka na kumuuwa mtoto Asimwe mshitakiwa namba moja ambaye ni  Padri Elipidius Rwegoshora aliwaambia washitakiwa wengine akiwemo Baba mzazi wa mtoto Asimwe kununua sumu ya panya na kukaa nayo mda wote ili wakikamatwa na polisi wanye sumu hiyo wafe kupoteza ushahidi.

Aidha aliwaambia pia kuwa wao baada ya kufa angetunza familia zao ambapo katika Maelezo ya onyo yaliyosomwa Mahakama hapo padri Elipidius alikana.

Katika kesi iyo jumla ya vyelelezo 37 vitatumika Mahakama kuu  wakati wa kusikiliza shauri hilo  vyelelezo 27 zikiwa ni nyaraka uku vyelelezo 10 ni vya kushikika.

Mahakama ya hakimu mkazi Bukoba Septemba 6, 2024 imefunga rasmi  mwenendo kabidhi (commital)  katika Mahakama hiyo na shauri hilo litaanza kusikilizwa katika Mahakama kuu kanda ya Bukoba.

Dkt. Biteko: Serikali haitapuuza mchango wa AZAKI
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 7, 2024