Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Kasim Majaliwa ameongoza mbio za hisani z Benki ya Maendeleo (Maendeleo Bank Marathon) zillizofanyika jijini Dar es salaam kwa lengo la kuchangia watoto waliozaliwa njiti katika Hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro na ujenzi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Dikonia kitakachojengwa wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.

Waziri mkuu aliunga mkono juhudi za Benki ya Maendeleo kwa kutoa jumla ya shilingi milioni 140 ziweze kutumika kwa wahitaji wa KCMC ambao walikabidhiwa hundi ya Shilingi milioni 80 na ujenzi wa kituo cha Dikonia waliokabidhiwa hundi ya milioni 60.

 

Washiriki kutoka taasisi mbalimbali za ndani na nje ya Dar es salaam waliibuka kidedea katika mashindano hayo yaliyohusisha mbio fupi za kilomita 2.5 ,km 5,km10 na mbio ndefu za km 21. wafanyakazi wa Kampuni ya DataVision International yenye ofisi zake Mikocheni jijini Dar es Salaam, wote waliibuka na  medali .

 

Mkoa wa Arusha uliongoza kwa kuwa na wakimbiaji wengi waliojinyakulia zawadi mbalimbali ukifuatiwa na Dar es salaam ,Mwanza na Njombe.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Septemba 8, 2024
Marathon: DataVision International wazoa medali, waacha gumzo