Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Justine Nyamoga imezitaka Halmashauri zote nghini kufanya tathimini na kuwatambua mahitaji ya kiasi kinachotakiwa kuwawezesha na walimu na wataala wa Afya wanaojitolea katika vituo vya kutolea huduma za Afya pamoja na shule zetu ilu kuona namna ya kuwawezesha.
Nyamoga ameyasema hayo katika kikao cha majumuisho ya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya afya, elimu na miundombinu inayotekelezwa katika Halmashauri ya wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Amesema Kamati inatambua uhaba wa Watumishi katika Halmashauri mbalimbali nchini hivyo watu wanaojitoalea kutoa huduma kwa Wananchi yafaa kupatiwa motisha kidogo ili kuongeza ari na uwajibikaji katika ufanyaji wao wa kazi.
Kamati hiyo, imefanya ziara na kukagua ujenzi wa shule mpya ya bweni ya Wasichana ya Mkoa iliyopo kata ya Mbigili inayojegwa kupitia mradi wa SEQUIP, ujenzi wa kituo cha afya Ilula, ujenzi wa kituo cha afya Nyalumbu, mradi wa kuondoa vikwazo katika barabara ya Ilula – Ilambo ambapo kamati imerizishwa na namna ambavyo miradi hiyo imetekelezwa.
Aidha Kamati imeitaka Serikali kuendelea kusimamia thamiani ya fedha katika utekelezaji wa Miradi mbalimbali kwa kuhakikisha inakua bora ambayo itaweza kudumu kwa muda mrefu na kutoa huduma kwa wananchi.
Akiongea kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Ofisi Rais TAMISEMI, Atupele Mwambene amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI imechukua maelekezo yote yaliotolewa na Kamati na itasimamia utekelezaji wake.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI imeanza ipo ziarani mkoani Iringa na imetembelea Miradi katika halmashauri ya Kilolo kisha itaelekea Halmashauri ya Mufindi na Mafinga.