Huenda unadhani kuna watu wanapenda sana Chai hii leo, lakini ukweli ni kwamba wao wamechelewa kuna watu waliipenda sana chai kuliko maisha yao, na ilifikia kipindi walikuwa wakificha au kufungia chupa za kinywaji hicho kwenye Masanduku.

Kwa waliowahi kusikia kisa cha Stuart na Georgia wa Nchini Uingereza watakuambia kwamba hali ilikuwa mbaya kipindi hicho, kwani Chai ilikuwa ikiagizwa kutoka Uchina na kwa hivyo ilikuwa ghali sana.

Na kwa muktadha huo, Chai ilikuwa ni anasa na ukionekana unainywa basi ulitafsiriwa kama wewe ni familia bora yenye kipato, kwani ni Matajiri pekee ndiyo walioweza kumudu hitaji hilo.

Ilikuwa ghali sana kwa kweli, kwamba masanduku maalum ya chai yalitengenezwa na kuwekewa kufuli juu, hivyo hakuna mtu anayeweza kuiba chai! na familia zingine alikodiwa mlinzi maalumu kulinda kinywaji hicho kwani hakuna mtu alitakiwa kuiona isipokuwa muhusika pekee.

Kama ungelikuwa mmoja wapo kwa kipindi hicho, nadhani hata wewe hungeliwaamini watumishi wako kukutengenezea kikombe japo kimoja kwa kuhisi ungezidiwa maarifa! lakini je, leo hii unaweza kufungia chai kwenye Sanduku?

Waswahili waliwahi kusema ‘Kipya kinyemi ingawa ni kidonda,’ kiukweli walikuwa na maana kwamba kitu hata kama ni kibaya lakini ni chako ukikihusudu, hivyo tusiwashangae kwa kuficha chai ila tuwe na kumbukumbu kwamba hakukuwa na Chai kipindi hiko kwani iliagizwa kutoka China pekee.

Kifo cha Kibao : Mwenye taarifa za uhakika aziwasilishe - Polisi
Nyamoga: Wataalamu wanaojitolea Halmashauri wawezeshwe