Boniface Gideon – Tanga.
Balozi wa Tanzania Nchini Uganda, Meja Generali Paul Simuli amesema kasi ya ujenzi wa mradi wa Bomba la Mafuta unaenda kwa kasi nakwamba utakamilika kwa wakati.
Balozi Simuli ameyasema hayo jana, wakati akihitimisha ziara ya kukagua miundombinu ya ujenzi wa Bomba la Mafuta ,kutoka Ohima Nchini Uganda hadi chongoleani Nchini Tanzania katika Gati la kupokelea Mafuta Bandari ya Tanga.
Balozi Simuli amesema namna ambavyo ametembelea Mradi huo katika maeneo yote kuanzia Nchini Uganda na Tanzania na ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo.
“Nimepita katika maeneo yote kuanzia Kagera hadi hapa Tanga, kiukweli nimeridhika na kazi, nimefika Handeni pale Misima nimekuta wameshaanza Kutandaza mabomba, hivyo, ukiangalia mpaka hapo utaona kabisa kuwa kasi ni kubwa sana, tunatarajia kuwa mradi wetu utakamilika kwa wakati,” alisema Balozi Simuli
Aliwataka makandarasi anayetekereza kipande cha Bomba hilo kwa Tanga pamoja na mkandarasi anayetekereza ujenzi wa Gati la kupokelea Mafuta katika Bandari ya Tanga,kuongeza kasi zaidi ili kufanikisha mradi huo kwa wakati,
“Niwaombe muongeze kasi zaidi ya hapa,kama walivyofanya pale Handeni,basi hata nyie nanyi pia nataka nione mkiwa kama Handeni,haiwezekani Handeni wamalize kazi alafu alafu hapa bado,ninayo imani kubwa na nyie na kwakasi hii lengo litatimia kwa wakati” Alisisitiza Balozi Simuli.
Kwaupande wao,Wakazi wa kata ya Chongoleani, walisema ujio wa mradi huo umewasaidia kupata ajira na kupunguza uhalifu mtaani,
Ally Mohamed mkazi wa kata ya Chongoleani na Mfanyabiashara wa matunda,alisema kwasasa vijana wengi kwenye kata yao wamepata ajira kutokana na mradi huo,
“Tunashukuru kiukweli, vijana wetu kwasasa wapo kazini,na wale ambao hawajaajiliwa wanafanya Biashara mana kwasasa kata yetu imeongezeka idadi ya watu kutokana na shughuli kuwa nyingi,hivyo tunashukuru kiukweli kwa mradi huu,” aliongeza Mohamed.