Mfululizo wa matukio ya utekaji na kuuawa kwa Wananchi, umepelekea baadhi ya Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – Chadema na ACT Wazalendo, wamewataka Waziri Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Camillius Wambura kuachia ngazi.

Hayo yamejiri hii leo Septemba 9, 2024 mkoani Tanga, wakati wa kutoa salamu kwenye msiba wa aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Ali Kibao.

Kibao, anadaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana kwenye basi la Tashrif Septemba 6, 2024 eneo la Kibo Complex Tegeta Mkoani Dar es Salaam akiwa safarini kuelekea Tanga na mwili wake kupatikana Septemba 8, 2024 eneo la Ununio.

Hata hivyo, wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni akihutubia wananchi kulitokea vurugu za raia ambao waliibua madai ya kumtaka ajiuzulu nafasi yake kutokana na matukio ya kutekwa Wananchi yanayozidi kushika kasi.

Hali hiyo, ilitulizwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kwa kuwaomba Wananchi hao kumuacha Waziri Masauni amalize hotuba yake.

Maisha: Ufinyanzi wa Ladi ulihamia kwenye noti
Balozi Simuli aridhishwa kazi ujenzi Bomba la Mafuta